• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mafuriko ya maji yasababisha vifo vya watu 280 Afrika mashariki

    (GMT+08:00) 2019-12-06 10:20:06

    Ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa ripoti kuwa, watu wasiopungua 280 wamefariki na wengine milioni 2.8 kuathiriwa katika mafuriko yanayoendelea kwa miezi kadhaa mfululizo katika eneo la Afrika mashariki.

    Ripoti hiyo imesema mvua kubwa inayonyesha nchini Kenya kuanzia mwezi wa Oktoba imesababisha vifo vya watu 132, na nchini Tanzania watu 50 pia wamefariki katika mafuriko.

    Ripoti pia imesema mvua kubwa bado zitaendelea ambapo hali ya mvua nchini Kenya, Tanzania na Uganda itakuwa mbaya zaidi. Uwezekano wa mlipuko wa kipindupindu na magonjwa mengine ya kuambukiza unaendelea kuongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako