• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachumi wapongeza uamuzi wa serikali ya Afrika Kusini wa kulinusuru Shirika la Ndege la nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-12-06 17:21:10

    Wachumi nchini Afrika Kusini wamepongeza uamuzi wa serikali ya nchi hiyo wa kulinusuru Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) linalokabiliwa na deni kubwa.

    Shirika hilo linalomilikiwa na serikali limewekwa chini ya mpango wa kunusuru biashara kufuatia mgomo wa siku saba ulioleta hasara kubwa ya kifedha mwezi uliopita, na kulilazimu kufuta safari za ndege za ndani na nje ya nchi hiyo.

    Profesa Jannie Rossouw wa kituo cha uchumi katika Chuo Kikuu cha Witwatersand jijini Johannesburg amesema, uamuzi huo lazima upongezwe kwani utainusuru kampuni hiyo kufilisiwa.

    Mara ya mwisho kwa Shirika hilo kupata faida ilikuwa ni mwaka 2011, na katika miaka iliyopita, lilitegemea msaada wa mabilioni ya fedha kutoka serikalini kuendesha shughuli zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako