• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uganda azindua kituo cha ukaguzi kwenye Eneo la Viwanda lililojengwa na China nchini humo

    (GMT+08:00) 2019-12-06 18:10:07

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezindua kituo ha ukaguzi katika Eneo la Viwanda la Liaoshen, katikati ya wilaya ya Nakaseke nchini humo.

    Kituo hicho ambacho kitakuwa na maofisa wa uhamiaji na mamlaka ya kodi, kinalenga kurahisisha biashara katika Eneo hilo. Rais Museveni amesema, sera ya utandawazi ya Uganda na mwingiliano wa soko la kikanda vimevutia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni nchini humo.

    Ameishukuru serikali ya China kwa kufadhili maendeleo ya miundombinu barani Afrika.

    Balozi wa China nchini Uganda Zheng Zhuqiang amesema, China imejikita katika utekelezaji wa Hatua Nane Kubwa zilizoitangazwa katika mkutano wa FOCAC uliofanyika hapa Beijing. Amesema, kwa kuwa Uganda inaharakisha mageuzi ya kiviwanda, China iko tayari kubadilishana uzoefu wake katika uzalishaji na usimamizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako