• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la al-Shabaab laua watu 10 katika mji wa Kenya ulio karibu na mpakani

    (GMT+08:00) 2019-12-07 17:10:45

    Takriban watu kumi wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kundi la al-Shabaab, jana jioni kuvamia basi la abiria kaskazini mashariki mwa Kenya.

    Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa kaunti ya Wajir Stephen Ngetich, kundi al-Shabaab lilivamia Basi la Medina lililokuwa likisafiri kutoka Nairobi kuelea Mandera na kuwaua wakristo waliomo ndani ya basi. Amesema tukio hilo limetokea katika eneo kati ya mji wa Wargdadud na Kutulu na kwamba hivi sasa basi lipo kituo cha polisi huku uchunguzi ukiendelea.

    Mashuhuda wamesema wageni au wakristo watatu wamefanikiwa kutoroka, mmoja akiwa hajadhuriwa. Ripoti za mwanzo zinaonesha kuwa wengi wa wahanga ni maofisa wa polisi waliokuwa wanarudi kwenye vituo vyao vya kazi huko Elwak na Mandera karibu na mpaka na Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako