• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa China kuunga mkono utafiti wa kijiolojia na rasilimali za madini wa Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-12-07 17:11:07

    Karibu wataalamu 120 wa China watajiunga kwenye mradi unaofadhiliwa na China wa tathmini ya utafiti wa kijiolojia na rasilimali za madini nchini Rwanda katika miaka mitatu ijayo na kikundi cha kwanza kimeshaanza kufanya kazi nchini humo.

    Mmoja wa wataalamu Liu Xiaoyang amesema Mradi huo unajumuisha mambo mbalimbali yakiwemo tafsiri ya kijiolojia ya satelaiti inayohisi mbali na kuweka ramani ya muundo wa kemikali ardhini kote nchini Rwanda, tathmini ya utafiti wa kijiolojia na rasilimali za madini, mafunzo ya kiufundi katika teknolojia ya utafiti wa kijiolojia n.k..

    Afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Migodi, Petrol na Gesi Francis Gatare amesema mradi huu ni muhimu kwa Rwanda katika Nyanja nyingi, ambao utaisaidia Rwanda kujua uwezo wa rasilimali za madini na jinsi watakavyotumia katika kubadilisha uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako