• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliokufa maji kwenye boti ya wahamiaji iliyozama pwani ya Mauritania yaongezeka

    (GMT+08:00) 2019-12-07 18:09:25

    Shirika la Uhamiaji la Kimataifa IOM jana lilitangaza kuwa idadi ya watu waliokufa maji katika ajali ya kuzama kwa boti ya uvuvi iliyokuwa imebeba wahamiaji wanaokwenda kisiwa cha Canary Jumatano iliyopita imeongezeka na kufikia 62 hadi Alhamisi jioni.

    Shirika hilo liliwaambia waandishi wa habari kuwa nahodha wa boti hiyo anadhaniwa kuwa miongoni mwa watu waliokufa na kulingana na mashuhuda, kuna wasiwsi kuwa idadi hiyo itaendelea kuongezeka.

    Shirika hilo pia lilisema kuwa sasa linashughulikia kuwasaidia wahamiaji hao kupona kutokana na ajali hiyo, kupata matibabu sahihi na kuchunguza afya zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako