• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali ya kuanguka kwa jengo Nairobi yafikia watano

    (GMT+08:00) 2019-12-08 17:19:55

    Idadi ya watu waliokufa kutokana na kuanguka kwa jengo mjini Nairobi imeongezeka na kufikia watano, wakati mamlaka zimeimarisha juhudi za usakaji na uokoaji.

    Kamishna msaidizi wa Kaunti ya Nairobi Bw. James Wanyoike amesema idadi ya watu wasiojulikana walipo imepungua kutoka 30 hadi 26, huku idadi ya waliookolewa imeongezeka na kufikia 33. Bw. Wanyoke amewaambia wanahabari kuwa kazi ya uokoaji kwenye jengo lililoporomoka lenye ghorofa sita katika eneo la Tassia mashariki mwa Nairobi bado inaendelea.

    Sekta ya nyumba nchini Kenya imekuwa ikikua kutokana na ongezeko la mahitaji ya nyumba, lakini ongezeko hilo limekuja na ongezeko la nyumba zinazobomoka wakati wa msimu wa mvua, kutokana na udhaifu kwenye sekta hiyo.

    Rais Uhuru Kenyatta ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike, na kutoa salamu za rambirambi kwa ndugu wa waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako