• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia na Umoja wa Mataifa waungana kutafuta suluhu ya kudumu ya msukosuko wa wakimbizi

    (GMT+08:00) 2019-12-08 17:20:21

    Serikali ya Ethiopia na wadau wa kibinadamu wamezindua mkakati wa taifa wenye lengo la kuweka mazingira mazuri kwa wakimbizi wa ndani.

    Mkakati huo wa suluhisho endelevu (DSI) uliotolewa na serikali ya Ethiopia, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kitaifa na kimataifa yasiyo ya kiserikali pamoja na wadau wengine, unalenga kuhakikisha wakimbizi wa ndani wanaweza kurudi, kujiunga na jamii au kuhamia sehemu nyingine kama wanavyopenda.

    Waziri wa amani wa Ethiopia Bw. Mufeirat Kamil amesema wanapenda wadau wa maendeleo kutilia maanani mambo yanayofuatiliwa na wakimbizi wa ndani na jamii zinazoathiriwa, kwenye mipango ya kuwasaidia.

    Mratibu mkazi na mratibu wa mambo ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ethiopia Bw. Steven Omamo amesisitiza kuwa mpango huo ni hatua muhimu kwenye kutimiza na kurudisha haki za wananchi walio kwenye shida, na kuwasaidia kujenga maisha yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako