• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliokufa kwa mafuriko magharibi mwa Uganda yafikia 17

    (GMT+08:00) 2019-12-09 08:54:15

    Polisi nchini Uganda wamesema hadi kufikia jana jumapili idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mafuriko ya ghafla magharibi mwa nchi hiyo, imefikia 17.

    Kamanda wa polisi wilaya ya Bundibugyo Bw. Swaibu Taban amesema miili sita zaidi ya wahanga imepatikana jana, na kuifanya idadi ya jumla ya miili iliyopatikana ifikie 17.

    Ofisa huyo pia amesema wamegundua eneo moja ambalo miili mingi zaidi ilifunikwa. Mafuriko hayo ya ghafla yalitokea kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwenye eneo la Bundibugyo na kusababisha mito mitatu kufurika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako