• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya waliokufa kwa ajali ya kuporomoka kwa jengo Nairobi yafikia kumi

    (GMT+08:00) 2019-12-09 09:14:06

    Idadi ya watu waliokufa kutokana na kuporomoka kwa jengo mjini Nairobi imeongezeka na kufikia kumi, miili mingine minne imepatikana katika operesheni ya utafutaji na uokoaji.

    Kamanda wa polisi mjini Noirobi Bw. Philip Ndolo amesema miili hiyo minne ni watoto wawili na mwanamume mmoja, na mwingine alikufa hospitali kutokana na kujeruhiwa vibaya. Hadi sasa miili kumi imepatikana kwenye kifusi. Ameongeza kuwa watu wengine wawili wameokolewa, na idadi ya watu waliookolewa imefikia 35, lakini bado kuna watu 11 wasiojulikana walipo.

    Kamishna wa msaidizi wa kaunti ya Nairobi Bw. James Wanyoike amesema kazi ya uokoaji inatarajiwa kumalizika Jumatatu, lakini inategemea hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako