• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 90 wauawa na wengine 90 kujeruhiwa kutokana na wanyamapori ndani ya mwaka mmoja nchini Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-12-09 09:42:44

    Watu zaidi ya 96 wameuawa na wengine 90 wamejeruhiwa kutokana na wanyamapori waliovamia mashamba na maeneo ya makazi nchini Tanzania kutoka Julai mwaka 2018 hadi Julai mwaka 2019.

    Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii ya nchi hiyo Bw. Adolf Mkenda amesema, idadi ya watu waliouawa na kujeruhiwa na wanyamapori imeongezeka ikilinganishwa na miaka iliyopita.

    Amesema hayo katika mkutano uliofanyika Mwanza kujadili njia bora za kudhibiti migongano kati ya binadamu na wanyamapori, huku akisema wanyamapori wamewaua watu 39 na kuwajeruhi wengine 37 kutoka Julai mwaka 2017 hadi Julai mwaka 2018.

    Ametaja tembo, simba, faru na mamba wamekuwa chanzo kikuu cha mauaji hayo, huku akiongeza kuwa kutoka mwaka 2018 hadi 2019, wanyama hao wameharibu hekta 13.644 za mazao mashambani ikilinganishwa na hekta 637 za mwaka 2017 hadi 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako