• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kushuka kwa uchumi wa Namibia kunachochea vitendo vya kujiua

    (GMT+08:00) 2019-12-09 19:37:02

    Mwanasaikolojia Shaun Whittaker kutoka nchini Namibia amesema, mgogoro wa kiuchumi wa nchi hiyo, ukosefu wa ajira na ukame vinaongeza hatari ya watu kutaka kujiua.

    Mwanasikolojia huyo amesema, kuna uhusiano wa wazi kati ya kushuka kwa uchumi na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaojiua, na kuongeza kuwa ni wazi ukosefu wa ajira ni sababu kubwa ya watu kujitoa uhai, wakati masuala mengine kama kutoridhika na mazingira ya sehemu za kazi kunachangia msongo wa mawazo. Amesema shinikizo binafsi kutokana na mgogoro wa kiuchumi linaweza kuwafanya watu wengine zaidi kuchukua hatua ya kujitoa uhai.

    Takwimu zilizotolewa na jeshi la Polisi nchini humo zinaonyesha kuwa, watu 373 walijiua katika miezi tisa ya mwanzo ya mwaka huu, na wengi wa watu waliojiua ni wanaume watu wazima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako