• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 12 wafariki na wengine 91 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2019-12-09 20:43:52

    Watu 12 wamefariki na wengine 91 kujeruhiwa baada ya lori lililobeba watu karibu 103 kupinduka katikati ya Nigeria.

    Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Niger Bw. Joel Dagwa amesema, ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sawmill, karibu na mkoa huo, na chanzo chake ni mwendo mkali wa dereva wa lori hilo lililokuwa likielekea Lagos.

    Ajali za barabarani zinatokea mara kwa mara nchini Nigeria, na mara nyingi zinasababishwa na kubeba mizigo mikubwa kupita kiasi, barabara mbovu, na uendeshaji mbaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako