• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kwanini baadhi ya wabunge wa Marekani wanataka kujifanya wao ni wasemaji wa magaidi?

  (GMT+08:00) 2019-12-10 08:55:03

  Filamu mbili za documentary zilizotangazwa hivi karibuni na kituo cha televisheni cha CGTN kilicho chini ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, zimeonesha wazi madhara yanayoletwa na ugaidi na itikadi kali kwa mkoa wa Xinjiang, na kuzusha mjadala mkubwa kwenye jumuiya ya kimataifa.

  Mbele ya ukweli huo, vitendo vilivyofanywa na baadhi ya wabunge wa Marekani vya kupotosha na kupaka matope sera za China za kuondoa ugaidi na itikadi kali mkoani Xinjiang na kutumia vigezo viwili kwa ugaidi na itikadi kali, vimedhihirisha kuwa wanajifanya kuwa wasemaji wa magaidi! Mienendo yao imekwenda kinyume na maadili ya kimsingi ya binadamu.

  Picha halisi zinazooneshwa kwenye filamu hizo mbili zinaisaidia jumuiya ya kimataifa kufahamu kwa kina chanzo cha suala la Xinjiang, na kuelewa ulazima na uhalali kwa serikali ya China kuchukua hatua za kupambana na ugaidi, pia zinaonesha wazi kuwa suala la Xinjiang sio suala la haki za binadamu, kabila au hata dini, bali ni suala la mapambano dhidi ya wafarakanishaji na magaidi. Mapambano dhidi ya ugaidi na itikadi kali mkoani Xinjiang kamwe hayahusiani na eneo maalumu, kabila maalumu au dini maalumu, bali yanatoa mchango mkubwa katika shughuli za kimataifa za kuondoa ugaidi.

  Tukio la shambulizi la kigaidi la Septemba 11 lililotokea nchini Marekani haliko mbali. China inawataka baadhi ya wabunge wasipoteze maadili yao ya kimsingi, na wasiwe kikwazo cha mapambano ya kimataifa dhidi ya ugaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako