• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa ACP watoa mwito wa kuanzisha mfumo wa pande nyingi ulio na nguvu kubwa

    (GMT+08:00) 2019-12-10 09:05:10

    Mkutano wa tisa wa kilele wa Afrika, Caribbean na Pasifiki (ACP) umefunguliwa Jumatatu huko Nairobi, na kutoa mwito wa kuanzisha mfumo wa pande nyingi ili kuhimiza biashara ya haki, ongezeko linaloshirikisha pande mbalimbali, amani na utulivu kusini mwa dunia.

    Wakuu wa nchi 17 na nchi 70 wanachama wa ACP wameshiriki kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

    Kwenye ufunguzi huo rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema, utaratibu wa dunia kwa msingi wa kanuni unatakiwa kuimarishwa, ili kuhimiza hatua za kukabiliana na changamoto kama umaskini, migogoro, siasa kali za kimabavu na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Rais Kenyatta amesema nchi za ACP zinatoa mwito wa kuanzisha mfumo wa pande nyingi ulio wa haki na usawa, ili kulinda uchumi wa nchi hizo kutokana na mazoea ya kibiashara yasiyofaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako