• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yakusanya maoni ya umma kuhusu kazi za serikali

  (GMT+08:00) 2019-12-10 19:05:07

  Pendekezo lililotolewa kwenye mtandao wa internet linaloitwa "Nataka Kuongea na Waziri" limezinduliwa na tovuti rasmi ya serikali kuu ya China na tovuti nyingine ili kukusanya maoni ya umma na mapendekezo kuhusu kazi za serikali.

  Maoni au mapendekezo kuhusu mada 20 ikiwemo kupunguza umaskini, mazingira ya biashara, ajira, elimu, huduma kwa wazee na kipato yanaweza kuwasilishwa kwenye tovuti hizo. Zoezi hilo litafanyika kuanzia leo hadi mikutano ya mwaka ya Bunge la Umma la China NPC na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC itakapofunguliwa mwanzoni mwa Machi mwakani.

  Maoni ya umma, yakiwa yanapewa umuhimu mkubwa, yatawasilishwa kwa mashirika yanayowajibika kuandaa "Ripoti kuhusu Kazi za Serikali".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako