• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapinga shutuma zisizo na msingi dhidi ya hali yake ya haki za binadamu

  (GMT+08:00) 2019-12-10 19:59:52

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying amesema China inapinga baadhi ya nchi kutozingatia hali halisi na badala yake kutoa shutuma zisizo na msingi dhidi ya hali ya haki za binadamu nchini humo.

  Akizungumza kwenye Siku ya Haki za Binadamu Duniani inayoangukia leo tarehe 10, Disemba, Hua amesema wananchi wa China wana haki zaidi ya kueleza ulinzi wa haki zao za kibinadamu ulivyo. Amesema serikali ya China inatilia maanani sana kuendeleza haki za binadamu, kutoa kipaumbele kwa maslahi ya wananchi, kuweka uwiano kati ya kanuni ya upatikanaji haki za binadamu kwa wote na hali halisi ya nchi, na kufanya haki ya kuishi na kupata maendeleo kuwa ni haki muhimu zaidi ya binadamu. Ameeleza kuwa katika miaka zaidi ya 70 iliyopita, chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, watu karibu bilioni 1.4 wamejitosheleza kwa chakula na wengine milioni 850 waliokuwa maskini wameondokana na umaskini. Ameongeza kuwa, China inazitaka nchi mbalimbali kuheshimu njia ya maendeleo ya haki za binadamu inayochaguliwa na nchi husika na inapenda kushirikiana na pande nyingine kuhusu mambo ya haki za binadamu katika msingi wa usawa na kuheshimiana na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako