• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa Jukwaa la Haki za Binadamu la Kusini-Kusini lafanyika Beijing

  (GMT+08:00) 2019-12-12 09:58:37

  Mkutano wa Jukwaa la Haki za Binadamu la Kusini-Kusini kwa mwaka 2019 umefanyika jana hapa Beijing. Mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, ambaye pia ni mkuu wa idara ya uenezi ya kamati kuu ya chama Bw. Huang Kunming, amehudhuria mkutano huo na kutoa hotuba kuhusu "kushikilia anuwai ya staarabu za binadamu, na kuhimiza maendeleo ya haki za binadamu duniani".

  Bw. Huang Kunming amesema, kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu ni mafanikio makubwa ya maendeleo ya staarabu za binadamu, na pia ni juhudi zinazofanywa na chama cha kikomunisti cha China na serikali ya China. Katika hali mpya, nchi zinazoendelea zinapaswa kushirikiana kulinda mazingira ya maendeleo ya haki za binadamu yenye amani na utulivu, kuvumbua mfumo wa aina mbalimbali wa kuendeleza haki za binadamu, kutafuta mustakabali wenye uwiano wa maendeleo ya haki za binadamu, kuboresha usimamizi wa haki za binadamu duniani wenye haki na usawa, ili kutoa mchango katika kuhimiza maendeleo ya haki za binadamu duniani na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako