• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu ya Uganda kutoharibu noti za nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-12-13 19:01:50

    Benki ya Uganda imewataka raia wa Uganda kukubali noti za pesa ilizozitengeneza pekee. Kauli hiyo inakuja wakati ambapo baadhi ya noti zimekuwa zikiharibiwa kwa kuandikwa jumbe mbali mbali na kusambazwa mitaani.

    Benki ya Uganda imesema hatua hiyo pia inafuatia kuwekwa kwa noti bandia ambazo zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii nyingine zikiwa na jumbe za kisiasa. Benki hiyo imesema ni hatia kuweka stampu, kuandika ama kuweka alama kwa noti yoyote ile kwa kuwa inaharibu sehemu muhimu za uthibitisho wa uhalali wa pesa ya nchi hiyo. Gavana mkuu wa Benki hiyo Bw Emmanuel Mutebile amesema ni jukumu la raia wa Uganda kuhakikisha kuwa fedha ya nchi hiyo inalindwa kwa kuzingatia muundo wake halisi. Amesema mtu yeyote atakayepatikana akiharibu noti ya pesa ya nchi hiyo atachukuliwa hatua kali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako