• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Patriots yatinga nusu fainali ya kufuzu BAL

    (GMT+08:00) 2019-12-19 14:08:31

    Timu ya Patriots ya Rwanda imesonga mbele kwenye nusu fainali ya mashindano yanayoendelea ya kufuzu Ligi ya Basketball Afrika (BAL) East Division ikiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya kushinda game zao mbili za mwanzo. Mabingwa hao wa Rwanda waliowatoa kijasho JKT ya Tanzania kwa 113-61 Jumanne wamejihakikishia nafasi yao katika nne bora kufuatia ushindi wa 76-53 dhidi ya UNZA Pacers ya Zambia Jumatano usiku katika uwanja wa ndani wa Kigali. Man of the match Kenneth Gasana ameshinda pointi za juu 24, huku Patriots wakiimarisha kampeni za kukutana na Mabingwa wa Madagascar GNBC katika nusu fainali leo Alhamisi. Katika mchezo mwingine wa Jumatano

    GNBC imeichabanga JKT ya Tanzania kwa 87-63, huku Ferroviario kutoka Msumbiji ikiiondoa City Oilers ya Uganda katika ushindi mwembaba wa 92-87. Kutokana na kushindwa JKT na UNZA Pacers wametoka kwenye michuano hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako