• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Cristiano Ronaldo aacha watu vinywawazi kwa muda aliokaa hewani na kufunga bao la kichwa

    (GMT+08:00) 2019-12-20 10:21:25

    Mchezaji hatari wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo aliwaacha wadau, mashabiki na wapenzi wa soka ulimwenguni vinywa wazi baada ya kufunga bao hatari na lililozua gumzo mitandaoni kwenye ushindi waliyopata wa magoli 2 – 1 dhidi ya Sampdoria Jumatano usiku. Ronaldo akifunga bao hilo dakika 45 za kipindi cha kwanza kupitia kichwa, na kuzua gumzo kutokana na umbali alioruka hewani mpaka kuupata mpira hali iliyopelekea kocha wa timu pinzani, Claudio Ranieri akikaririwa akisema kuwa kwenda hewani kule na kuchukua muda mrefu mpaka kurudi chini ni 'Style za NBA' akimaanisha ndiyo wachezaji pekee wanao ruka juu mno wakati wakitaka kuingiza mpira wavuni. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, kupitia bao hilo anafikisha jumla ya magoli 10 akiwa wa pili kwenye mbio za kuwania ufungaji bora Serie A nyuma ya Ciro Immobile mwenye magoli 17.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako