• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Bandari ndogo ya Kabwe yakamilika asilimia 85

    (GMT+08:00) 2019-12-23 19:18:16

    Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini Tanzania (TPA), imesema imefikia asilimia 85 ya ujenzi wa bandari ndogo ya Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

    Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Percival Salama, aliyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ziara ya kukagua shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na TPA.

    Salama alisema bandari hiyo ni ya kisasa na itakuwa ya pili kwa ukubwa kwa mkoa huo baada ya Bandari ya Kasanga na kwamba itakuwa mkombozi wa usafiri wa maji katika ziwa hilo.

    Mhandisi wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Nyakato Lwamnana, alisema Bandari ya Kabwe ni kitovu cha biashara kati ya Mkoa wa Rukwa na mikoa mingine pamoja na nchi jirani.

    Alibainisha kuwa mradi huo unahusisha ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 74 kuingia majini, jengo la abiria, ghala, nyumba za watumishi, jengo la mgahawa na uzio utakaozunguka eneo lote la bandari pamoja na ujenzi wa barabara ya mita 600 kutoka eneo la bandari hadi nje ya bandari hiyo.

    Alisema mradi huo ukikamilika, utaongeza ufanisi wa huduma za bandari hiyo na kuingiza mapato zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako