• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Maandalizi ya Riadha Taifa Ngorongoro yakamilika

  (GMT+08:00) 2019-12-25 18:03:53

  Maandalizi ya mashindano ya Taifa ya riadha yanayotarajiwa kufanyika jumamosi na jumapili kwenye Chuo cha Elimu ya Taifa Butimba, jijini Mwanza, yamekamilika. Michuano ya mwaka huu inajulikana kama "Mashindano ya Riadha ya Taifa Ngorongoro 2019" yanatarajiwa kushirikisha wanariadha kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Riadha Tanzania imesema, kwa kutambua wajibu wa michezo katika kuchangia maendeleo ya taifa, ikiwamo kuitangaza nchi na vivutio vya utalii, imeamua kuyapa mashindano hayo jina hilo kwa kuheshimu ushirikiano unaofanywa na Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako