• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali kulipa madeni ya wanakandarasi

  (GMT+08:00) 2019-12-25 18:08:33

  Kaimu Waziri wa Fedha Ukur Yatani ametoa hakikisho kwamba Serikali ya Kitaifa imejitolea kulipa madeni inayodaiwa na wanakandarasi na wafanyabiashara.

  Bw Yatani alisema Serikali ya Kitaifa inadaiwa jumla ya Sh58.2 bilioni. Kati ya pesa hizo Sh43.2 bilioni ni madeni ambayo uhalali wake unabishaniwa na ambayo yanafanyiwa ukaguzi na uchunguzi.

  Madeni ya kima cha Sh43.2 bilioni ambayo uhalali wake unabishaniwa yamewasilishwa kwa kamati maalum shirikishi (Multi Agency Team) ambayo Rais Uhuru Kenyatta aliamuru ibuniwe, alipoongoza mkutano wa baraza la mawaziri wiki jana.

  Kulingana na Waziri Yatani, baadhi ya mashirika ya serikali kuu na serikali za kaunti zimekuwa zikisusia kulipia bidhaa na huduma inazopewa na sekta ya kibinafsi. Kuhusu serikali za kaunti, Waziri Yatani alisema kwa ujumla zinadaiwa Sh22.71 bilioni ambazo zimethibitishwa kuwa halali.

  Ukaguzi maalum ambao ulifanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufikia Juni 30, 2018 unaonyesha kuwa serikali za kaunti zinadaiwa jumla ya Sh88.98 bilioni, ambapo Sh51.2 bilioni zimethibitishwa kuwa halali. Kufikia Jumatatu Desemba 23 Hazina ya Kitaifa ilikuwa imetoa jumla ya Sh112.04 bilioni kama fedha za mgao wa fedha katika bajeti ya kitaifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako