• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Seikali ya Kenya yaahidi kulipa madeni yake

  (GMT+08:00) 2019-12-26 19:59:24

  Kaimu Waziri wa Fedha Ukur Yatani ametoa hakikisho kwamba Serikali ya Kitaifa imejitolea kulipa madeni inayodaiwa na wanakandarasia na wafanyabiashara.

  Kwenye taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari mapema wiki hii, Bw Yatani alisema Serikali ya Kitaifa inadaiwa jumla ya Sh58.2 bilioni. Kati ya pesa hizo Sh43.2 bilioni ni madeni ambayo uhalali wayo unabishaniwa na ambayo yanafanyiwa ukaguzi na uchunguzi.

  Madeni ya kima cha Sh43.2 bilioni ambayo uhalali wayo unabishaniwa yamewasilisha kwa kamati maalum shirikishi (Multi Agency Team) ambayo Rais Uhuru Kenyatta aliamuru ubuniwe, alipoongoza mkutano wa baraza la mawaziri wiki jana.

  Kulingana na Waziri Yatani, baadhi ya mashirika ya serikali kuu na serikali za kaunti zimekuwa zikidinda kulipia bidhaa na huduma inazopewa na sekta ya kibinafsi.

  Kuhusu serikali za kaunti, Waziri Yatani alisema kwa ujumla zinadaiwa Sh22.71 bilioni ambazo zimethibitishwa kuwa halali.

  Ukaguzi maalum ambao ulifanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufikia Juni 30, 2018 unaonyesha kuwa serikali za kaunti zinadaiwa jumla ya Sh88.98 bilioni, ambapo Sh51.2 bilioni zimethibitishwa kuwa halali.

  Hii ni kwa sababu madeni ya kima cha Sh37.7 bilioni zinakosa stakabadhi za kuonyesha kuwa bidhaa au huduma ziliwasilishwa au kazi ilifanywa. Na hivyo, hazijathibitishwa kulipwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako