• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Rashford ajifananisha na Ronaldo baada ya kufunga goli la kichwa dhidi ya Newcastle

  (GMT+08:00) 2019-12-27 17:12:14

  Mchezaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Marcos Rashford ameamua kutoa ya moyoni na hisia zake baada ya kufunga goli la kichwa dhidi ya Newcstle United. Mchezo huo ambao ulichezwa katika uwanja wa Old Trafford, Manchester United walifanikiwa kupata ushindi wa goli 4-1 liccha ya kutoka nyuma baada ya Newcastle kutangulia kupata goli. Ushindi huo wa United unaifanya kusogea hadi nafasi ya 7 wakiwa na alama 28 kwenye msimamo wa ligi. Goli la Rashford dakika ya 41 ndio ambalo limemfanya kuongea maneno yote hayo na kujihisi anataka kumfikia Cristiano Ronaldo aina yake ya ufungaji. Ikumbukwe hii sio mara ya kwanza Rashford kufananishwa na Ronaldo kwani katika mchezo wa Chelsea dhidi ya United katika kombe la Carabao alifunga goli la freekick ambalo mchezaji mwenzake wa United raia wa Sweden Lindelof alisema kuwa hili goli kama nishawahi kuliona kabla huku akipost picha ya Ronaldo akifunga goli kama hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako