• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba ya Mkuu wa CMG kwa ajili ya Sikukuu ya Mwaka mpya

    (GMT+08:00) 2020-01-01 16:02:31


    Tarehe 1 Januari mwaka 2020, mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG Bw. Shen Haixiong alitoa hotuba ya mwaka mpya kwa wasikilizaji walioko ndani na nje ya nchi kupitia Radio China Kimataifa CRI na mtandao wa Internet, yafuatayo ni yaliyomo ya hotuba yake:

    Marafiki wapendwa,

    2020 ni nambari yenye bahati na neema, kwani watumiaji wa mtandao wa Internet wa China wanalinganisha nambari hii na maana ya "kukupenda". Wakati mwaka mpya wa 2020 unapowadia, ningependa kutoa salamu za mwaka mpya kwa wasikilizaji wetu popote pale mlipo duniani kwa niaba ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, na kuwatakia furaha na kila la heri!

    Historia ya binadamu inaundwa na nyakati mbalimbali, na zile za mwaka 2019 zimewekwa kama ni kumbukumbu zinazohifadhiwa daima. Tarehe 1, Oktoba, tulisherehekea kwa shangwe Miaka 70 tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Ninyi marafiki zetu mmeangalia filamu iliyoonyesha hali halisi ya "tukipiga hatua barabarani" ambayo inatengenezwa kwa lugha mbalimbali za kigeni na CMG, na filamu ya aina ya 4K iliyotangazwa moja kwa moja iitwayo "Gwaride kubwa la mwaka 2019" , na kufahamu mchakato usio wa kawaida wa miaka 70 tangu kuanzishwa kwa China mpya. Vilevile nimepata salamu za dhati kutoka kwa marafiki wengi. Mtaalamu wa Italia anayeshughulikia masuala ya China Bw. Francesco Maringio amesema kupitia barua pepe kuwa, "Ningependa kusifu mafanikio yaliyopatikana katika miaka 70 iliyopita tangu China mpya ilipoasisiwa. Naona kuwa wananchi wa China wanastahili kuona furaha na kuionea fahari nchi yao."

    Katika mwaka uliopita, tumekuwa tukijitahidi kuweka kumbukumbu kuhusu kila wakati unaong'ara wakati China inaposonga mbele, ili kuonesha China halisi na kwa pande zote ambayo iko katika zama mpya kwa dunia nzima. Tulitumia teknolojia ya 5G na 4K/ 8K na akili bandia, kuripoti shughuli mbalimbali kubwa zikiwemo Mkutano wa Baraza la Kilele la Ushirikiano wa Kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", Mkutano wa mazungumzo kati ya staarabu za Asia, pamoja na maadhimisho ya miaka 20 tangu Macao irudi China. Vipindi maalumu vya lugha za kigeni tulivyoviandaa kuhusu "Nukuu za kifasihi anazopenda Rais Xi Jinping" , na "Endapo hazina ya taifa inaweza kuongea" , vimefungua madirisha kwa marafiki zetu kufahamu kwa kina utamaduni na historia ndefu za China pamoja na mtazamo wa thamani ya China katika zama mpya; shughuli za wasikilizaji duniani "Kusonga mbele kwa pamoja na China", shughuli za uvumbuzi za vyombo vya habari vya aina zote kati ya China na Russia, na watangazaji wa lugha mbalimbali wanaofurahisha kwenye mtandao wa Internet, pia zimewavutia watu wengi kuwa "mashabiki" wa China.

    Ingawa ni miaka miwili tu tangu kuanzishwa kwa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, lakini tumejua wazi kwamba tukiwa kwenye zama ya mtandao wa Internet, tutarudi nyuma bila ya kupata maendeleo hata kupata maendeleo taratibu. Tunapaswa kukumbuka vizuri maagizo aliyotoa rais Xi Jinping kuhusu "kufanya uvumbuzi kwa kufuata kanuni ya kimsingi ya maendeleo, na kujenga na kutumia vizuri vyombo vya habari vya aina mpya na majukwaa mapya", kushikilia kutoa kipaumbele uvumbuzi, na kupiga hatua kwa kasi kubwa katika kujengwa kuwa chombo kikuu cha habari cha aina mpya chenye kiwango cha juu cha kimataifa. Mwaka huu, tumezindua ujenzi wa maabara muhimu ya kipekee yenye uwazi zaidi ya utengenezaji na utangazaji ya video na audio, kujenga manowari ya vyombo vya habari vipya vya video na audio inayoweza kudhibitiwa kwa kujitegemea---"Yangshipin" ambayo ni jukwaa la chombo cha habari kwa njia ya video cha 5G; kuzindua kwa pande zote marekebisho ya vipindi yenye ubora wa hali ya juu, kutangaza vipindi bora zaidi ya 200, ili kuandaa vipindi vinavyowafurahisha na kuwavutia watumiaji zaidi.
    Kutangaza masuala muhimu duniani kwa pande zote, mtizamo wa kuzingatia ukweli wa mambo na haki, ni kanuni tunazozifuata. Tunachukua msimamo wazi na ushirikiano, kufanya mawasiliano yenye usawa na wenzi wetu nchini na nje ya nchi. Mwaka huu, nimefanya mawasiliano na wakuu wa vyombo vya habari vya nchi zaidi ya 150 likiwemo shirika la habari la Marekani AP, la Ufaransa AFP, na la Uingereza BBC, na tumepata makubaliano mengi zaidi na kupata marafiki wengi zaidi.

    Lakini wakati huo huo pia nimesikitika kwa kuona kuwa, kutokana na sababu zisizoeleweka, baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi zimeonekana kuwa upofu kwa machaguo kwenye baadhi ya ripoti zinazohusu China, hata zinazitangaza uvumi kuwa habari, na kupotosha ukweli wa mambo, baadhi ya ripoti zimebadilika kuwa habari za kubuniwa. Sote tunaona kuwa ukweli wa mambo ni roho ya ripoti ya habari, kutangaza ripoti kwa kutegemea kukisia, au kutunga habari kama ni hadithi, itaathiri vibaya chombo chochote cha habari. Hayo vilevile yanatakiwa kututahadharisha wakuu wa vyombo vya habari vinavyobeba majukumu ya kazi.
    Mwandishi wa Uingereza wa karne ya 18 William Hazlitt ana msemo maarufu: "Upuuzi ni matunda ya ujinga." Inathaminiwa sana kwa kutafuta ukweli wa mambo na kuondoa upendeleo! Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG itaendelea kufuata msimamo wenye mtizamo wa haki, kueneza ukweli wa mambo na haki kwa jumuiya ya kimataifa.
    Mshairi wa enzi ya Tang wa China Zhang Jiuling aliwahi kusema: "Kufahamiana bila ya kujali umbali, na kuwa majirani hata wakitengwa kwa umbali mkubwa." Ni bahati kwetu kwa kuishi na kukutana kwenye sayari hii. Kama nilivyofanya ziara nchini Brazil na Argentina, nilifurahia kuona maua ya Jacaranda na Bougainvillea na kusikia sauti ya ndege wa Catbird kama nilivyozisikia mkoani Guangdong nilipofanya kazi huko. Katika nchi za Italia na Hispania, nilionja pamoja na waandishi wa habari wenzangu divai ya mchele unaonata na nyama ya wanyama kama walioko nyumbani kwetu mkoani Zhejiang. Hili kweli ni wazo la "Kijiji cha dunia"! Hakuna sababu kwa watu wanaoishi kwenye "kijiji" hiki kutowasiliana na kutoingiliana. Siku zote nashikilia kuwa mawasiliano kati ya vyombo vya habari yanasaidia kuondoa tofauti na upendeleo na kuwawezesha watu wengi zaidi kufanya marafiki.  
    Mwaka 2020 utakuwa muhimu katika kutimiza kuijenga China iwe jamii yenye maisha bora, pia kutimzia nchi hii yenye idadi ya watu bilioni 1.4 kutokomeza kabisa umaskini ambayo haijaonekana katika historia ya binadamu. CMG itarekodi zama hii kwa mtizamo wa kutafuta usahihi na ubora wa hali ya juu, kuwafahamisha marafiki wote hadithi nyingi zaidi zinazotokea nchini China na dunia nzima, ili kuingiza nguvu kwa wingi zaidi katika kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
    Mwaka 2020, uijaze upendo dunia ya binadamu!
    Tunaitakia China, dunia na wewe kila la heri!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako