• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Tanzania, Sudan Kusini na Ethiopia zatemwa na Caf kwenye orodha ya marefa

  (GMT+08:00) 2020-01-02 08:43:53

  Wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) likitoa orodha ya awali ya waamuzi 29 watakaofanyiwa mchujo kwa ajili ya kuchezesha Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (Chan), hakuna refa wa Tanzania katika orodha hiyo. Mashindano hayo ya Chan ambayo yatafanyika Cameroon kuanzia Aprili 4 hadi 25 yatashirikisha timu za taifa za nchi 16 huku Tanzania ikiwa ni miongoni mwao. Katika orodha hiyo ya waamuzi 29 iliyotolewa na CAF, ni Tanzania, Sudan Kusini na Ethiopia ambazo marefa wake hawajapata fursa ya kuwemo katika uteuzi wa mwanzo huku nchi nyingine wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) zikibahatika kwa waamuzi wao kuwemo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako