• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Cristiano Ronaldo aanza mwaka kwa kishindo kwa kupata hat-trick yake ya kwanza kwenye ligi ya Serie A

  (GMT+08:00) 2020-01-07 10:32:35

  Cristiano Ronaldo jana alifunga hat-trick yake ya kwanza katika mwaka huu kwenye ligi ya Serie A na kuipaisha juu Juventus kwenye msimamo wa ligi baada ya kupata ushindi wa 4-0 dhidi ya Cagliari huku Zlatan Ibrahimovic mambo yakimwendea kombo kwani alionekana kutotosha mboga katika klabu yake ya AC Milan kwa kuanza mechi yake ya kwanza akiondoka kapa ambapo walitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Sampdoria. Mshambuliaji wa Ureno Ronaldo ameshinda mechi ya tano mfululizo ya ligi na kujisogeza nyuma ya Inter Milan. Ronaldo mwenye miaka 34 amesema anafurahia hat-trick hiyo lakini jambo muhimu Zaidi ni timu yake ambayo imecheza vizuri, alisisitiza kuwa iliwalazimu kushinda ili kuipa presha Inter

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako