• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Abiria wote waliokuwa ndani ya ndege iliyoanguka ya Ukraine wamethibitishwa kufariki

  (GMT+08:00) 2020-01-08 16:03:12

  Abiria wote na wafanyakazi waliokuwa kwenye ndege aina ya Boeing 737 ya Ukraine ambayo ilianguka karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomenei mjini Tehran, Iran, wamethibitishwa kufariki.

  Msemaji wa Uwanja huo wa ndege Ali Kashani ameliambia Shirika la Habari la Iran kuwa, ndege namba PS-752 ilikuwa na abiria 167 na wahudumu tisa wakati ilipoanguka wilayani Parand, kusini mwa Tehran.

  Ndege hiyo ni mali ya Kampuni ya Ndege ya UIA ya Ukraine, iliyokuwa inaelekea Kiev, ilianguka dakika chake baada ya kupaa.

  Wakati huohuo, Shirika la Habari la Interfax la Ukraine limeripoti kuwa rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine ametoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa ajali hiyo.

  Vilevile China imetoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa ajali hiyo na kutarajia chanzo chake kijulikane mapema iwezekanavyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako