• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Simba, Azam FC kukutana nusu fainali Mapinduzi Cup

  (GMT+08:00) 2020-01-08 16:50:26

  Mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la Mapinduzi timu ya Azam FC na Simba zimeungana na Mtibwa Sugar kuingia nusu fainali ya mashindano ya kombe hilo. Azam FC ilitinga hatua hiyo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mlandege uwanja wa Amaan juzi usiku, mchezo ambao ulikuwa mkali na kupendeza kwa muda wote. Mchezo mwengine wa kundi B uliosukumwa kwenye dimba la Gombani Pemba, baina ya timu ya Simba na Zimamoto, mchezo ambao ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1. Katika mchezo huo Simba ilianza kwa kasi ikisaka bao la mapema na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya nne lililofungwa na John Boko. Simba iliendelea kuliandama lango la Zimamoto na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya nane, lililofungwa na Sharaf Shiboub. Simba waliweza kutumia vyema nafasi walioipata dakika ya 54 kuandika bao la tatu lililofungwa na Ibrahim Ajib.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako