• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya Dunia yasema uchumi wa dunia unatarajiwa kukua kwa asilimia 2.5 mwaka 2020

  (GMT+08:00) 2020-01-09 08:38:04

  Benki ya Dunia imesema ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka huu unakadiriwa kufikia asilimia 2.5, ikilinganishwa na asilimia 2.4 ya mwaka jana, licha ya kuendelea kuwepo kwa hatari ya kushuka.

  Ripoti mpya kuhusu mustakbali wa uchumi wa dunia inayotolewa kila baada ya nusu mwaka na Benki ya Dunia, inasema ongezeko hilo linaweza kuwa kubwa zaidi kama hatua za kisera zinazochukuliwa hivi karibuni, haswa zile ambazo zimepunguza mvutano wa kibiashara, zitaendelea kupunguza sintofahamu ya sera.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ukuaji katika masoko yanayoibuka na nchi zinazoendelea unatarajiwa kufikia asilimia 4.1 mwaka 2020 kutoka asilimia 3.5 ya mwaka 2019, huku ukuaji katika nchi zilizoendelea ukikadiriwa kushuka hadi kufikia asilimia 1.4 kwa mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 1.6 ya mwaka jana.

  Uchumi wa China unakadiriwa kukua kwa asilimia 5.9 mwaka huu, ukipungua kutoka asilimia 6.1 ya mwaka 2019.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako