• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza na Ujerumani zasisitiza juhudi za kulinda makubaliano ya nyuklia ya Iran

    (GMT+08:00) 2020-01-13 09:23:12

    Uingereza na Ujerumani zimesisitiza juhudi zao za kushikilia makubaliano ya nyuklia ya Iran bila kujali shinikizo kutoka kwa Marekani.

    Msemaji wa ofisi ya waziri Mkuu wa Uingereza amesema, waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Boris Johnson na chansela wa Ujerumani Angela Merkel wamejadili kwa njia ya simu maslahi ya pamoja katika kuhakikisha Iran haiwezi kupata silaha za nyuklia, na kusisitiza juhudi zao za kuendelea na makubaliano ya JCPOA.

    Msemaji huyo pia ameongeza kuwa, wakuu hao wawili pia wamejadili hali ya Libya na umuhimu wa kufanya mazungumzo na washirika wa kimataifa na wa kikanda, ili kupunguza mvutano na kuhimiza msaada kwa mchakato unaoongozwa na Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako