• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiongozi wa Hezbollah aapa kulipiza kisasi kuuawa kwa kamanda wa Iran

  (GMT+08:00) 2020-01-13 10:07:15

  Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah amesema kutakuwa na operesheni mbalimbali dhidi ya vikosi vya Marekani katika kanda ya mashariki ya kati, ili kulipiza kisasi Marekani kuwaua makamanda wa Iran na Iraq mapema mwezi huu.

  Bw. Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba ya televisheni kwa ajili ya kukumbuka wiki moja ya vifo vya mkuu wa Kikosi cha Quds cha Iran Qassem Soleimani, na kamanda wa wanamgambo wa Iraq Abu Mahdi al-Muhandis. Amesema Marekani haina chaguo lingine ila kuwaondoa wanajeshi wake kwa hiari, au kurudisha miili yao katika majeneza nchini mwao. Bw. Nasrallah pia amekanusha madai ya Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Bw. Soleimani kuwa na mipango ya kushambulia ubalozi wa Marekani. Aidha, Bw Nasrallah ameisifu Iran kwa ujasiri wake wa kushambulia vikosi vya jeshi la Marekani nchini Iraq.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako