• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe na China zinatakiwa kuchukua hatua za kiuvumbuzi kudumisha ushirikiano wa pande mbili

    (GMT+08:00) 2020-01-13 16:32:44

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Zimbabwe amesema, nchi hizo mbili zinatakiwa kwenda na kasi ya wakati, na kuchukua hatua za kivumbuzi ili kuufanya ushirikiano na uhusiano wa pande mbili kuwa endelevu.

    Wang Yi ambaye pia ni mjumbe wa taifa la China, amesema hayo alipokutana na waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa wa Zimbabwe, Sibusiso Moyo. Katika mazungumzo yao, Bw. Moyo amesema chini ya maelekezo ya viongozi wa nchi hizo mbili, ushirikiano wa kimakakati wa pande zote kati ya China na Zimbabwe umeendelea kuimarika. Amesema Zimbabwe inavutiwa na mafanikio ya maendeleo ya China, na kuishukuru nchi hiyo kwa mchango wake wa muda mrefu kwa maendeleo ya uchumi na jamii nchini Zimbabwe.

    Kwa upande wake, Wang Yi amesema China iko tayari kushirikiana na Zimbabwe kuendelea kuunga mkono kila upande katika masuala yanayohusiana na maslahi ya pande hizo mbili. Pia amesema, China itaiunga mkono kithabiti Zimbabwe katika maendeleo yake ya uchumi na jamii. Wang amesema, China iko tayari kufanya uratibu na kushirikiana na Zimbabwe katika masuala ya pande nyingi na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako