• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvutano kati ya Marekani na Iran yatasababisha kuongezeka kwa bei ya petroli katika eneo la Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2020-01-13 17:07:38

    Gazeti la Business Daily la nchini Kenya limesema, kutokana na Marekani kumuua kamanda wa Iran na kusababisha kuongezeka kwa hali ya wasiwasi kwenye sehemu ya Mashariki ya Kati, wastani wa bei ya mafuta ghafi iliongezeka kutoka dola za kimarekani 65.5 kwa pipa ya mwezi Desemba mwaka jana, hadi dola za kimarekani 72.01 kwa pipa, kiasi ambacho kimefikia kiwango cha juu zaidi tangu mwezi Mei mwaka jana.

    Nchini Tanzania, Gazeti la Daily New limeandika, baada ya kuongezeka kwa hali ya wasiwasi kati ya Marekani na Iran, watanzania wana wasiwasi kuwa bei ya mafuta nchini humo inaweza kuathiriwa. Kutokana na hali hiyo, serikali ya Tanzania imetangaza kuchukua msimamo chanya juu ya utulivu wa bei ya mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako