• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watumiaji milioni 22 wa simu nchini Tanzania bado hawajasajili kadi za simu kwa alama za vidole

    (GMT+08:00) 2020-01-14 09:30:01

    Wakati Januari 20 ambayo ni tarehe ya mwisho ya usajili wa kadi za SIM za simu za mkononi kwa alama za vidole nchini Tanzania inakaribia, bado kuna kadi 22,796,000 ambazo hazijasajiliwa.

    Ofisa mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyanjala amesema hadi kufikia Januari 7, takriban kadi 25,160,000 za SIM sawa na asilimia 52.4 ya kadi zote zinazotumiwa zilikuwa zimesajiliwa. Amesema TCRA inatarajia kwamba kadi nyingi zaidi zinaweza kusajiliwa katika siku saba zijazo hadi tarehe ya mwisho ya Januari 20.

    Tarehe 27 Desemba mwaka jana Rais John Magufuli wa Tanzania alirefusha tarehe ya mwisho ya usajili wa kadi ya SIM kwa siku 20, badala ya tarehe 31, Desemba mwaka jana.

    Madhumuni ya usajili wa kadi ya SIM kwa alama za vidole ni kuwatambua watumiaji wasioaminika, na kukabiliana na uhalifu wa kimtandao, ili kuwalinda Watanzania dhidi ya wale wanaotumia vibaya sekta ya simu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako