• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Namibia yapiga marufuku kuagiza matunda yenye wadudu kutoka Zambia

    (GMT+08:00) 2020-01-14 09:49:38

    Wizara ya Kilimo, Maji na Msitu ya Namibia imepiga marufuku kuagiza maembe yanayoshukiwa kubeba wadudu aina ya inzi wa matunda kutoka nchi jirani Zambia na eneo la Zambezi, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Ofisa wa habari wa Wizara hiyo Bw. Jona Musheko amesema marufuku hiyo inalenga kulinda bidhaa zinazouzwa nje ya nchi hiyo kama zabibu, matikiti maji, karanga na mboga. Wizara ya Kilimo imesisitiza kuwa katika siku za nyuma, mashaka yoyote juu ya bidhaa zinazouzwa Ulaya husababisha soko la bara hilo kukataa bidhaa kutoka Namibia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako