• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA:Barcelona yamtimua kocha wake Ernesto Valverde na nafasi yake kumpa Quique Setien

  (GMT+08:00) 2020-01-14 10:23:17

  Barcelona imemtimua kazini kocha wake Ernesto Valverde na nafasi yake kumpa kocha wa zamani wa Real Betis Quique Setien. Valverde, mwenye miaka 55, ameisaidia klabu kutwaa mataji mawili mfululizo ya La Liga na katika msimu huu wanaogoza kwa tofauti ya magoli. Hata hivyo upande wa Catalan umekuwa ikitoa sababu nyingi kuhusiana na uongozi wake na pia ameshindwa kufikia fainali ya Champions League. Setien, mwenye miaka 61, aliiongoza Betis na kumaliza katika nafasi nzuri tangu 2005 na kuipaisha hadi nusu fainali za Copa del Rey kabla ya kuondoka mwezi Mei. Kocha huyu amekubali mkataba wa miaka miwili na nusu. Kwenye taarifa yao Barca imesema wamefikia makubaliano na Valverde kukatiza mkataba wake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako