• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNAIDS yampongeza kiongozi wa Uganda kwa mapambano dhidi ya UKIMWI

    (GMT+08:00) 2020-01-15 09:25:42

    Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa Bibi Winnie Byanyima amempongeza rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa mchango wake katika mapambano dhidi ya UKIMWI nchini humo.

    Bibi Byanyima amesema Rais Museveni ameongoza juhudi katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kuhimiza kampeni ya utambuzi wa ugonjwa huo nchini humo. Mkuu huyo wa UNAIDS amekutana na rais Museveni katika jengo la bunge huko Entebbe kilomita 40 kusini mwa mji mkuu wa Kampala. Bibi Byanyima ameihimiza Uganda kufanya juhudi katika kufikisha ujumbe wa kinga ili kuhakikisha mapambano hayo yanafanikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako