• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamia ya watu wapoteza makazi katikati ya Tanzania kutokana na mvua kubwa

    (GMT+08:00) 2020-01-15 09:31:47

    Mamia ya watu kwenye wilaya ya Bahi katika mkoa wa Dodoma, wamepoteza makazi yao baada ya nyumba zisizopungua 120 kuanguka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

    Mkuu wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda amesema nyumba nyingi zimeharibiwa kwenye maeneo ya Bahi Sokoni, Bahi Misheni, Mji Mpya na Nkongwa na vijiji vya Mbuyuni, Uhelela, Laloi, Mugu na Nagulo.

    Ofisa huyo amesema serikali ya wilaya ya Bahi imeomba shilingi milioni 400 kutoka kwa serikali kuu ili kukarabati madaraja yaliyosombwa na mvua.

    Wiki iliyopita mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alisema mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwenye Nyanda za Juu Kusini zimesababisha vifo vya watu watatu na kusomba madaraja manne, na kukwamisha mawasiliano ya barabarani kwenye maeneo matatu jirani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako