• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Russia yajiuzulu baada ya rais Putin kuhutubia bunge

    (GMT+08:00) 2020-01-16 08:50:27

    Ofisi ya habari ya Ikulu ya Russia Kremlin imesema waziri mkuu wa Russia Bw. Dmitry Medvedev ametangaza kujiuzulu kwa serikali yake, baada ya rais Putin kulihutubia bunge la nchi hiyo.

    Hotuba hiyo ya mwaka inayoweka malengo na majukumu ya nchi, inakuwa mwongozo kwa serikali na bunge.

    Waziri mkuu Medvedev amesema rais Putin ametaja mabadiliko mbalimbali ya kimsingi kwenye hotuba yake, kwa hiyo serikali ya Russia inapaswa kumpatia rais fursa ya kufanya maamuzi yote yanayowezesha mabadiliko hayo.

    Mara baada ya kujiuzulu kwa serikali, rais Putin amemteua Bw. Medvedev kuwa naibu mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Russia, na kumteua aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Kodi Bw. Mikhail Mishustin kuwa waziri mkuu mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako