• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa ujasusi wa Sudan ajiuzulu baada ya kikosi cha usalama kuasi

    (GMT+08:00) 2020-01-16 08:50:50

    Mwenyekiti wa Baraza la utawala la Sudan ametangaza kujiuzulu kwa mkuu wa Shirika Kuu la Ujasusi la Sudan GIS jana Jumatano, siku moja baada ya uasi kutokea kwenye kikosi cha usalama kilicho chini ya GIS.

    Bw. Abdel Fattah al-Burhan ametoa tangazo hilo kwenye mahojiano na Televisheni ya Taifa ya Sudan, akisema mkurugenzi mkuu wa GIS Bw. Abu-Bakr Dambalab amekabidhi ombi la kujiuzulu, na ombi hilo linajadiliwa.

    Kikosi hicho kilichoasi pia kilifunga mistari ya uzalishaji kwenye moja ya maeneo ya mafuta magharibi mwa Sudan, kabla ya hali kudhibitiwa na maeneo mawili ya mafuta kutwaliwa tena na jeshi la Sudan. Serikali ya Sudan imelitaja tukio hilo kama "uasi" wa kikosi cha usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako