• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya asema ugaidi bado changamoto kubwa

    (GMT+08:00) 2020-01-16 08:55:13

    Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Dk. Fred Matiang'i amesema ugaidi bado ni changamoto kubwa nchini Kenya na hatua madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa ili kuepusha mashambulizi ya kigaidi.

    Waziri Matiang'i amesema kuanza upya kwa mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa na kundi la Al-Shabaab ni matokeo ya pengo kati ya kupeana taarifa za kijasusi na polisi jamii. Akiongea mjini Mombasa na maofisa usalama, Waziri Matiang'i amesema operesheni ikifanyika hakutakuwa na tofauti kati ya magaidi na wale wanaowahifadhi.

    Pia amewakumbusha viongozi wa mashinani kuimarisha ufuatiliaji na kutoa ripoti kuhusu watu wanaotia shaka kwa kituo cha kupambana na ugaidi.

    Wito huo umetolewa wakati Kenya inakumbuka mwaka mmoja wa shambulizi la kigaidi katika eneo la kibiashara Dusit mjini Nairobi, lililosababsha vifo vya watu 21.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako