• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Filipe Nyusi aapishwa kuwa rais wa Msumbiji kwa kipindi cha pili

    (GMT+08:00) 2020-01-16 09:10:17

    Bw. Filipe Nyusi ameapishwa kuwa rais wa Msumbiji kwa kipindi cha pili, na kusisitiza kuwa atahimiza maendeleo ya uchumi na amani ya taifa.

    Sherehe ya kuapishwa kwa rais Nyusi imeshirikisha wakuu wa nchi 12, vikundi vya kidiplomasia na maelfu ya wageni. Kwenye hotuba yake, rais Nyusi ameeleza malengo ya serikali yake kuhimiza maendeleo kwenye sekta za uchumi na jamii.

    Rais Nyusi amesema katika miaka mitano ijayo, amani itakuwa jambo la kipaumbele na serikali yake itaendelea kuhimiza amani kama hitaji la kwanza la maendeleo.

    Vilevile amesema, serikali yake itaboresha mazingira ya kibiashara, kupambana na ufisadi, na kuhimiza kilimo ili kuondoa njaa, kuongeza utoaji wa umeme, na kuhimiza utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako