• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Msakataji mzee wa kabumbu duniani Kazuyoshi Miura asaini mkataba mpya na Yokohama FC

    (GMT+08:00) 2020-01-16 12:32:22

    Msakataji mzee wa kabumbu duniani Kazuyoshi Miura amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na Yokohama FC utakaoshuhudia akiendelea kuvalia daluga zake hadi atakapofikisha umri wa miaka 53. Miura ni mshambuliaji wa kati kutoka Japan ambaye alizaliwa Februari 26 mwaka 1967 mjini Shizuoka. Klabu ya Yokohama itashiriki Ligi Kuu nchini Japan mwaka 2020 baada ya kupata tiketi kwa kumaliza Ligi ya Daraja la Pili katika nafasi ya pili nyuma ya Kashiwa Reysol anayochezea Mkenya Michael Olunga mwaka 2019. Miura, ambaye jina lake la utani ni King Kazu, alichezeshwa mara tatu pekee ligini msimu uliopita ikiwemo katika mechi ya Yokohama ya kufunga msimu dhidi ya Ehime FC alipoingizwa katika nafasi ya Yusuke Matsuo, mwenye miaka 22, dakika ya 87. Dakika tatu alizopewa katika mechi hiyo zilidhaniwa kama mechi yake ya kuwaaga mashabiki wake, lakini sasa atakuwa kikosini Ligi Kuu ya Japan itakapoanza mwezi ujao wa Februari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako