• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kagera Sugar yaingamiza Yanga kwa mabao 3-0

    (GMT+08:00) 2020-01-16 12:32:48
    Mshambuliaji wa Kagera Sugar Yusuph Mhilu jana alikiongoza kikosi chake kuingamiza Yanga kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru. Mhilu alifungua akaunti ya mabao dakika ya 13 kwa kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango Farouk Shikalo. Yanga ikiwa chini ya nahodha wao Haruna Niyonzima, ilimshuhudia kiungo wao Mohamed Issa 'Mo Banka' akiwapunguzia kasi dakika ya 44 baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa kuwachezea faulo wachezaji wa Kagera Sugar. Kipindi cha kwanza Yanga walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0 walijipanga kurejea kupindua meza kipindi cha pili mambo yakazidi kuwa magumu kwani Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime ilimzidi ujanja Luc Eymael ambaye ni mara yake ya kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi akipokea kijiti cha Mwinyi Zahera. Bao la pili kwa Kagera Sugar lilifungwa dakika ya 66 kupitia kwa Ally Ramadhan aliyemalizia pasi ya Abdallah Siseme na msumari wa mwisho ulipachikwa kwa kichwa dakika ya 89 na kuifanya Yanga kushindwa kutumia dakika nne za nyongeza kupata bao la kufutia machozi. Kagera Sugar inafikisha jumla ya pointi 27 na kupanda mpaka nafasi ya nne, huku Yanga ikiwa nafasi ya nane na pointi 25 kibindoni.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako