• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Manchester United yawa kileleni kwa uingizaji wa mapato katika klabu za England watatu katika klabu zote

    (GMT+08:00) 2020-01-16 12:33:45

    Miamba ya soka ya Premier League, Manchester United imeendelea kuwa kileleni kwenye maswala ya uingizaji wa mapato ngazi ya klabu England. United imezidi kuwa moto wa kuotea mbali mbele ya miamba mingine ya soka ya Premier League zikiwemo Manchester City na Liverpool ambazo zikiwa nyuma ya mashetani hao wekundu. United imeingiza kiasi cha pauni milioni 627.1 msimu wa mwaka 2018/19 na kuwafanya kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa klabu nyuma ya wafalme wa soka wa Hispania Barcelona wenye pauni milioni 741.1 wakiwa nafasi ya kwanza na Real Madrid pauni milioni 667.5 wakiwa wa pili katika jarida hilo. Manchester United imeonekana kuwa vizuri katika mapato licha ya klabu hiyo kushindwa kutwaa taji la ligi kwa muda sasa. United imekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu katika mkwanja ndani ya English tangu kuanzishwa kwa mfumo wa kuangazia uingizaji wa mapato kwa klabu 'Deloitte's Football Money League'

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako