• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Iran ailaumu Ulaya kwa kushindwa kuheshimu makubaliano ya amani ya suala la nyuklia la nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2020-01-16 16:46:11

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ameilaumu Ulaya kwa kushindwa kutimiza ahadi zao chini ya Makubaliano ya Pande zote ya Mpango wa Nyuklia wa Iran (JCPOA) yaliyofikiwa mwaka 2015.

    Amesema Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, ambazo ni nchi tatu zilizosaini makubaliano hayo, zinadai kuwa Ulaya imetimiza wajibu wake chini ya makubaliano hayo, hata hivyo, kiuhalisia, nchi hizo hazijanunua mafuta kutoka Iran na pia hazijawezesha utendaji wa kimataifa wa benki za Iran.

    Bw. Zarif amezialumu nchi hizo kwa kukubali shinikizo la Marekani dhidi ya kutimiza ahadi zake kwa Iran.

    Jumanne wiki hii, nchi hizo za Ulaya zilisema kuwa zinachukua hatua za kujibu kitendo cha Iran kutotimiza ahadi zake za makubaliano hayo katika miezi kadhaa iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako