• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kusainiwa kwa makubaliano ya kibiashara ya awamu ya kwanza kati ya China na Marekani ni maendeleo mazuri katika kutatua mgogoro

    (GMT+08:00) 2020-01-16 17:03:59

    Hafla ya kusaini makubaliano ya kibiashara ya awamu ya kwanza kati ya China na Marekani imefanyika jana kwenye Ikulu ya Marekani.

    Akizungumzia hatua hiyo, mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa mambo ya biashara, serikali na jamii ya Washington Bw. James Moor amesema, kusainiwa kwa makubaliano hayo ni maendeleo mazuri katika kutatua mvutano huo, na utaleta athari nzuri kwa nchi hizo mbili na kwa dunia. Amesema pande zote mbili zinapaswa kuendeleza majadiliano ya ana kwa ana.

    Amesema, "Naona kwamba, mazungumzo kati ya China na Marekani ni jambo muhimu kwa pande zote mbili siku zote. Nchi hizo mbili zinafanya juhudi ya kufikia makubaliano pamoja na kutatua masuala na changamoto zinazozikabili, kitendo ambacho ni kupiga hatua muhimu na kupata maendeleo mazuri kwa kuelekea upande sahihi."

    Amesema kuongeza ushuru kunaweza kuathiri pande zote mbili, na makubaliano hayo yanalingana na maslahi ya pamoja ya watu wa nchi mbili, pia yatailetea dunia athari nzuri. Hata hivyo, matokeo ya makubaliano hayo yanatokana na utekelezaji wa pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako